Pages

Tuesday, October 2, 2012

Serikali mnaiona barabara ya kwamnyamani?

Kwamnyamani ni miongoni mwa vitongoji vinavyounda kata ya buguruni, kwa bahati nzuri mtaa wa kwamnyamani umekuwa ukikua siku baada ya siku kwa kasi kubwa lakini sina uhakika kama serikali imeligundua hili au haijajua..miaka kadhaa iliyopita serikali iliona umuhimu wa barabara hii na kuiboresha mpaka kufikia kiwango cha lami lakini matunzo na maendelezo ya mtaa yamekuwa duni kama yapo au hamna kabisa kwani ukiangalia barabara imekuwa na mashimo mengi yasiyokarabatiwa nayayodaiwa kusababishwa na magari makubwa yanayoshusha nafaka katika maduka yaliyopo kando ya barabara na magari makubwa ya maji taka yanayopita kuelekea kumwaga taka hizo.Kama hiyo haitoshi barabara hii ni nyembamba sana hivyo kusababisha magari na waenda kwa miguu kupita kwa shida na muda mwingine kusasbabisha ajali zinazogharimu maisha ya raia wasio na hatia, ata hivyo pembezoni mwa barabara hiyo kumekuwa na ujenzi wa majengo ya biashara ya bei ghali kitendo kinachoonesha kwamba serikali haina mpango wa kuipanua barabara hiyo kwani itabidi ilipe fidia kubwa kwa wamiliki wa majengo hayo kitu ambacho kingeweza kuepukika. Kama hujajua barabara ya kwamnyamani ni njia mbadala kwa wakazi wa vingunguti ukiachilia barabar ya Nyerere na kwa baadhi ya wakazi wa tabata ukiachilia mbali barabara ya mandela.
                            zifuatazo ni picha nilizobahatika kuzipata za mtaa wa kwa mnyamani:

                                                         mashimo barabarani


                                                        ...mashimo barabarani



                                                        kwamnyamani rd


                                                 vyombo vinapata shida kupishana


                                                               kwamnyamani rd


                                                          kwamnyamani r.d


                                                       ..kwamnyamani r.d


                                                        kwamnyamani


                                           ghorofa linalokarbia kukamilika pembezoni mwa
                                           barabara ya kwamnyamani.

   
                                                   maduka kwamnyamani


                                                  kwamnyamani r.d

0 comments:

Post a Comment