Saturday, October 20, 2012
TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT
"Wapendwa Katika Bwana, Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla. Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina. Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu: Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33). Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini. Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo: Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake. Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga. Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo: Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili. Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa. Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi. Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama: Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi? Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma, Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii. Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo. Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu? Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie. Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine. Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).
Daima tukumbuke kuwa,
“KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” (Waefeso 6: 12).
Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu"
Sunday, October 14, 2012
Fake phones to be blocked soon.
TANZANIA will join her neighbour Kenya in getting rid of counterfeit telephone handsets in the country by switching them off.
Speaking to “Sunday News’ the
Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Acting Corporate
Communication Manager Mr Semu Mwakyanjala said the regulatory authority
is first planning to educate the public on the need to buy genuine
mobile phones.
“It is a long term plan to switch off
counterfeit mobile phones in operation, for now we are only focusing on
educating the public into buying genuine mobile phones,” Mr
Mwakyanjala noted. He said the move will eventually be taken by all the
other East African Member states, including Rwanda, Uganda and Burundi.
The Uganda Communications Commission
(UCC) was recently quoted as to saying that counterfeit gadgets will be
switched off at the end of November this year. A survey conducted by New
Vision in Uganda showed that mobile phone dealers in Uganda are feeling
the pinch as customers no longer want to purchase the ‘Made in
China’ phones believing most of Chinese phones are fake.
Mr Mwakyanjala said the aim of blocking
the counterfeit mobile phones is to boost security, noting that for the
exercise to work, the regulatory authority depends on cooperation of all
stakeholders in the communication industry. Explaining the software
used for blocking counterfeit phones,
Mr Issac Mruma from TCRA Consumer
Affairs department said the Central Equipment Identification Registrar
(CEIR) is employed to identify fake mobile phones and then block them.
Mr Mruma said the country is in the process of acquiring the software,
however it will only be implemented after the public is aware of the
advantages of genuine mobile phones.
Although Mr Mwakyanjala said the
initiative to switch off fake mobile phones was agreed on in a meeting
of the East African Communication Organization (EACO). The Rwanda
Utilities Regulatory Authority (RURA) was also quoted saying that it
will soon announce the date for switching off the fake mobile phones.
RURA said it is working on the
methodology to disconnect fake phones off their network and they will
work with telecommunication companies to execute the exercise. RURA
noted that it will use the International Mobile Equipment Identity
(IMEI) number through network service providers to differentiate between
fake and genuine handsets.
In Tanzania early this month the deputy
minister for Communication Science and Technology Mr January Makamba was
quoted in a local daily saying that the country is working out plans on
how to deal with fake handsets in light of Kenya’s move to switch
them off. Mr Makamba said the fear is that those fake phones from Kenya
will flood the Tanzania market, promising to convene a meeting with TCRA
to deliberate on the issue.
Reliable sources that declined to be
named had noted that Telecom service providers are reluctant for
government to institute the move to switch off all fake mobile phones,
for fear of losing customers.
However, recently Vodacom Tanzania
Managing Director Mr Rene Meza was quoted saying that the move is
commendable since it is aimed at protecting consumers’ rights and
heavy investments made by multination companies. TCRA is participating
in the Financial Service and Investment exhibition week at Mnazi Mmoja
grounds, where it is giving presentations to small and medium
entrepreneurs on financial issue.
source: dailynews
Friday, October 12, 2012
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA AUAWA NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO.
Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha kuuwawa kwa kakamnda wa Mwanza Liberatus Barlow .
Amesema kuwa kamanda huyo wa polisi ameuwawa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30 na saa 8 usiku katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.
Mwema amesema kuwa kamanda Barlow alikuwa akitokea katika kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla alikutwa na tukio hilo la kupigwa risasi.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linataraji kuanza uchunguzi wake kuanzia leo na timu ya askari kutoka makao makuu ya polisi wataondoka mapema leo kwenda jijini Mwanza kuungana na askari wa mkoa huo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na msako wa majambazi hayo .
Mwema amewataka wananchi wa Mwanza kutoa ushirikiano wao kwa jeshi la polisi ili kufanikisha zoezi hilo na kuwataka kutokuwa na hofu yoyote kutokana na tukio hilo.
Thursday, October 11, 2012
HOW TO GET RID OF YOUR PIMPLES
Desperate to know how to get rid of a Pimple overnight! Well, there are various natural as well as conventional remedies that tend to heal Pimples as soon as possible. Read further and discover ways on how to get rid of Pimples overnight.
• Ice is often used as a quick remedy to get rid of Pimple overnight. You just need to wrap an ice cube (or crushed ice) in a piece of cloth and apply it on your Pimple for about 20-30 seconds.
Repeat this procedure a few times in a day to reduce the swelling of your Zits considerably as it helps to freeze the pores and removes dirt and oil easily. If you are looking for solutions on how to get rid of a red Pimple fast then this ice remedy will surely give the best results.
• Manuka honey and tea tree oil also serve as excellent home remedies to get rid of Pimples overnight Apply either of these natural cures after washing the face. This treatment, however, works best in case of minor Pimples.
• Using any white toothpaste (not gel) on the Zits is quite a popular home treatment for this problem nowadays. For this, you simply have to apply some toothpaste on the Pimples before bed time and let it remain on the face over night. Wash your face the next morning and you will find a great deal of improvement in your Pimples. The toothpaste should remain on the Zits for at least half an hour.
Wondering how does Colgate toothpaste get rid of Pimples? This mint based toothpaste usually dries out Pimples and hence heals them quickly. Another tip as to how to get rid of a red Pimple overnight would be to use the ice remedy (mentioned earlier) after following this toothpaste remedy. Do not use this remedy in case your skin is sensitive as it may cause a burning sensation.
• If you are wondering how to get rid of a Pimple on your nose or forehead then lemon juice can be a great help for you. In fact, applying lemon juice on the affected area is one of the simplest ways of curing Pimples.
Just apply some fresh lemon juice on your Pimple before going to bed and let it dry overnight. Your Zits and Pimples would surely become much less noticeable or even disappear completely the next day.
• Consider using a honey and cinnamon face mask to mask your Pimples. Prepare this face mask by mixing some honey and cinnamon powder to form a sticky paste.
Then, apply this mixture on the face overnight and wash it off in the morning. However, this pleasant smelling mixture takes might take an unpleasant amount of time to treat Acne.
How to get rid of a Zit overnight using over-the-counter medicines?
• Acne products that contain benzyl peroxide and salicylic are highly recommended for curing this Acne and Zits. Read the instructions carefully before going ahead with these products. Do not over apply these products and follow the directions cautiously. Clearasil and Noxzema are quite popular in this regard.
• If acne products fail to give desired results and you are still intent on finding out how to get rid of Acne overnight then you can also try sulfur masks. Try not to leave a sulfur mask on your face overnight unless specifically mentioned.
Other Suggestions
Make sure you wash your face before applying these Acne and Pimple remedies. Although, do not become obsessed with face cleaning activity as washing the face too frequently can make the skin excessively dry.
In fact, learn to wash your face gently before learning how to get rid of pimples in a day. Just clean the skin two to three times in a day with a mild soap or a specialized Acne cleaner. After washing gently pat dry the skin instead of rubbing it vigorously.
In addition, do not squeeze or pop your Zits as it will only make the condition worse. As different individuals have different types of skin, the effectiveness of these remedies also varies from one individual to another.
Moreover, if you are seriously looking for an effective cure to get rid of Acne then you also need to follow a more holistic approach, especially in case of severe Acne breakouts.
Therefore these steps on getting rid of Pimples and Zits fast should also be accompanied by certain dietary measures like including more vitamin A and vitamin C rich foods in the diet, drinking adequate amount of water, avoiding highly sugary foods, etc.
RONALDO agreeS €15M-a-year contract
Cristiano Ronaldo has settled terms with Real Madrid over a new contract.
Terra says negotiations have reached a positive conclusion which will see Ronaldo extend his deal from 2015 to 2017 and see his wages jump from €10 million-a-year to €15 million-a-year.
The new agreement sees the former Manchester United star move into second place on the football earners' table, ahead of PSG striker Zlatan Ibrahimovic on €14.5 million-a-year, but still behind Anzhi's Samuel Eto'o on €20 million-a-year.
Ronaldo is delighted with the new agreement, which could be confirmed after the international break.
THE VAMPIRE DIARIES SEASON PREMIERE IS TONIGHT
ELENA’S WORST NIGHTMARE - Elena awakens on the morning after the
accident to find the thing she dreaded most has come true - she died
with vampire blood in her system and now must go through the terrible
transition to become a vampire…or face certain death. Stefan promises
Elena that he and Bonnie will exhaust every possible way out of the
situation, but Damon is furious with his brother for letting Elena die
in the first place. Bonnie pays a terrible price for her attempt to
change Elena’s fate, while Damon takes out his frustration and rage on
Matt. In a rare moment of empathy, Rebekah (guest star Claire Holt) is
deeply touched by Stefan and Elena’s devotion to one another. Finally,
Pastor Young (guest star Michael Reilly Burke) and the Town Council
members begin rounding up the vampires and their supporters, leading to an unexpected tragedy. Steven R. McQueen, Candice
Accola, Michael Trevino and Joseph Morgan also star. Chris Grismer
directed the episode written by Caroline Dries.
Season 4 released pictures
Season 4 released pictures
Subscribe to:
Posts (Atom)














